Kitabu cha mafunzo ya Uamsho wa Kijinsia kinaelezea kwa uwazi dhana mbalimbali zinazohusiana na jinsia na namna zinavyotumika katika jamii. Mafunzo ya jinsia yanalenga kuwawezeshawashiriki wa mafunzo kuelewa namna mahusiano ya kijinsia yanavyofanyika na kuonekana katika maisha ya kila siku ya kila mmoja wetu. Aidha mafunzo haya vilevile yanalenga kuleta mtizamo mpya wa mabadiliko ya kifikra na tabia kuhusu mahusiano ya kijinsia hususan kwa washiriki na jamii zetu kwa ujumla.
Kitabu cha Mafunzo ya Uamsho wa Kijinsia kinajenga mihimili ya kuendesha uamsho wa kijinsia katika taasisi mbalimbali na makundi mbalimbali katika jamii.
Malengo ya Mafunzo.
Ifikapo mwisho wa mafunzo haya washiriki waweze :-
JINSI ( SEX)
Jinsi ni maumbile yanayotofautisha kati ya mwanamke na mwanaume. Maumbile haya mtu anazaliwa nayo na hakuna anayechagua kuzaliwa mwanamke au mwanaume.(unicef:1990:5) Tofauti za kimaumbile kati ya watu hawa zinaonyesha kwamba mwanamke anao uwezo wa kubeba mimba, kujifungua (kuzaa) na kunyonyesha (maziwa au matiti yake mwenyewe) vitu ambavyo mwanaume hawezi kuvifanya. Japo sasa hivi katika nchi zilizoendelea wana sayansi wanajaribu kubadilisha maumbile haya kwa njia za upasuaji, kwa kawaida maumbile hayabadiliki.
JINSIA.( GENDER )
Jinsia ni mahusiano ya kijamii yanayotambua wavulana na wasichana , wanawake na wanaume wamelelewa katika misingi tofauti kufuatana na tabia, mila, desturi, utamaduni na matarajio ya jamii husika. Mahusiano ya kijinsia yanajengwa kwa njia ya kuelekeza au kufundisha yaani makuzi na malezi au kwa mtu kujifunza. Kwa hali hiyo , mahusiano ya kijinsia yaliyojengeka vilevile yanaweza kubadilika au kubadilishwa.
KAZI ZA KIJINSIA. ( Gender Roles)
Katika kujenga mahusiano ya kijinsia, jamii mbalimbali zimefanya mgawanyo wa kazi katika misingi ya kazi za wanawake nakazi za wanaume . Kwa mfano , kadri watoto wa kike wanavyokua , ndivyo wanavyolelewa na kufundishwa waweze kufanya kazi zinazodhaniwa ni za wanawake kama vile kazi za nyumbani ( kupika, usafi wa nyumbani, kulea wadogo zake ) na kazi nyingine nyingi zinazodhaniwa kuwa ni za wanawake.
Wavulana wamekuzwa kwa kufundishwa kufanya kazi zinazofanywa na wanaume au kazi zinazodhaniwa kuwa ni za wanaume, kwa mfano kazi za kuchunga mifugo, kuwinda na kazi nyingine nyingi ambazo jamii ilizitenga kuwa ni kazi za wanaume. Mgawanyo wa kazi kijinsia baina ya wanawake na wanaume umesababisha kuwepo na kazi za kijinsia za wanawake na wanaume.
Mgawanyo wa kazi kijinsia umegawanyika katika kazi zifuatazo:-
KAZI ZA UZAZI.
Kazi za uzazi zimeangaliwa katika mapana ya aina mbili.
KAZI ZA UZALISHAJI MALI.
Hizi ni kazi zinazofanywa na wanawake na wanaume (wasichana na wavulana) ili kuwawezesha kupata kipato ili waweze kuishi. Kazi za uzalishaji mali zinaingiza kipato au zinachangia nguvu kazi ambayo haijathamanishwa kwa kipato. Kiuchumi, kazi za uzalishaji mali zinapata malipo ya kifedha au zinachangia matumizi ya familia na kuziwezesha familia kuishi. Kitaifa, kazi za uzalishaji mali zinazoleta pato la kifedha zinaonekana kuchangia katika ukuaji wa pato la kitaifa. Lakini kazi za nyumbani zinafanywa na wanawake , zinawezesha familia nyingi sana kuweza kuishi bila kuwa mzigo mzito kwa serikali hazijapewa thamani inayostahili na hazihesabiwi kuchangia katika pato la taifa. Mara nyingi wanaume na wavulana hawapendi kuhusishwa na kazi za nyumbani.
KAZI ZA KUJITOLEA KATIKA JAMII.
Kazi hizi zinafanywa na wanawake na wanaume, zinajumuisha shughuli mbalimbali kwenye ngazi ya ujirani, mtaa, kijiji au jamii. Kazi hizi ni pamoja na kazi za maendeleo kama vile kukarabati barabara, kujenga shule, kuchimba visima vya maji, kusafisha soko la kijiji n.k. Vilevile kushiriki katika shughuli katika ujirani aidha za harusi au misiba na kadhalika.
Mara nyingi katika shughuli za kujitolea wanawake wanahusika kwa karibu sana kufanya kazi zinazodhaniwa kuwa ni za wanawake zinazofanywa nyumbani.Wanaume nao wanafanya kazi zinazoendana na kudhaniwa ni za wanaume . Kwa mfano -katika kazi za kujenga shule, wanawake watasomba maji, wanaume watafyatua tofali. Katika shughuli za harusi na misiba - wanawake watashughulikia masuala ya upishi wa chakula wakati wanaume wanakaa vikao vya kufanya maamuzi kuhusiana na nini kifanyike.
Iwapo katika kazi za kujitolea kuna baadhi ya shughuli zitatoa malipo kama kazi za ujenzi, ufundi n.k. mara nyingi wanaume au wavulana hunufaika kwa vile wengi wao wamefanikiwa kupata stadi zinazohitajika ikilinganishwa na wasichana au wanawake.
MAHITAJI YA KIJINSIA.
Wanaume, wanawake, wavulana na wasichana wakiwa ni binadamu kila mmoja wao ana mahitaji muhimu . Mahitaji haya yanajumuisha chakula, mavazi, makazi, upendo, urafiki, usalama, maji, elimu na starehe. Aidha inaeleweka wazi kwamba wanawake na wanaume wana majukumu tofauti na wanafanya kazi zinazotofautiana kulingana na mgawanyo wa kazi na majukumu ya kijinsia kwa sababu wanatofautiana katika kazi wanazozifanya vilevile mahitaji yao hutofautiana, kwa mfano , wanawake wana mahitaji yanayowawezesha kubeba ujauzito kwa hali iliyobora na ya salama, kujifungua kwa usalama na kupewa misaada yote muhimu wakati wa kujifungua , kipindi chote anachonyonyesha mtoto anastahili apate bora na maziwa mengi yenye virutubisho vinavyotakiwa ili lishe ya mtoto iwe nzuri. Kwa mfano suala zima la uzazi salama linahitaji lishe bora , kupimwa kliniki ya uzazi, kupata huduma hiyo karibu, kupimwa maradhi mengine ili yatibiwe mapema n.k.
Mwanamke na mwanaume mkulima wanahitaji nyenzo na rasilimali zitakazowezesha kilimo chao kiweze kuwa cha manufaa; kuchangia pato lao wenyewe na pato la taifa kwa ujumla n.k.
Mahitaji ya kijinsia yapo aina mbili :-
Mahitaji yanayolenga kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi yoyote ile mtu anayofanya Mahitaji haya yanatokana na kazi zinazofanyika kila siku katika suala zima la kazi zinazolenga kukimu familia na kuongeza ufanisi katika uzalishaji mali n.k.
Mahitaji mbinu yanalenga kuleta mageuzi na mabadiliko katika mfumo wa maisha uliopo ili wanawake na wanaume wawe kwenye nafasi sawa. Mahitaji haya yanataka kubadilisha kabisa mfumo uliopo sasa ambao ni wa ukandamizaji, uonevu na unyanyasaji dhidi ya wanawake; na kutokomeza ukandamizaji na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya wanawake, hali ambayo imejengeka kwenye mila na desturi , tabia, imani, taasisi, sera na sheria mbalimbali za nchi hii na duniani kote. Kwa mfano, kuwapa miliki ya ardhi na rasilimali zingine zote wanawake kama ilivyo kwa wanaume; kuwawezesha wanawake kama ilivyo kwa wanaume kupata elimu na mafunzo ya upeo wa juu, kuondoa aina zote za ukatili na ubaguzi dhidi ya wanawake na wasichana . Kwa sababu mfumo wa ubaguzi wa kijinsia umejengeka kwa vizazi vingi, mabadiliko ya mahitaji mbinu hayawezi kufanyika kwa urahisi . Inabidi kuanza uamsho wa kubadili fikra na mawazo ; kuwawezesha wanawake na wanaume kuelewa kwamba ubaguzi wa kijinsia unajengwa na jamii na unaweza kubadilishwa vilevile. Aidha kujenga uwezo wa wanawake kujiamini , pia kuimarisha mashirika au vyama vya wanawake vinavyoshughulika na masuala ya kijinsia ili kujenga mshikamano na kutandaa kwa madhumuni ya kushinikiza mabadiliko haya yafanyike. Ili kupata mafanikio yapatikane , inabidi wanawake wawe kama chachu inayouma mikakati ya kuleta mabadiliko. Hatima ya mahitaji mbinu ni kuwazesha wanawake kuwa kwenye nafasi na hadhi iliyo katika mstari mmoja na wanaume katika jamii zetu na pia kujenga uwezo wa wanawake na kuleta mageuzi ya jamii kwa ujumla.
Kujirudia kwa tabia kijinsia. (Gender Stereotype)
Kuendeleza tabia na matendo ya wanawake au wanaume inaonyesha wazi namna ambavyo fikra na mazoea ya binadamu vimejengeka kwenye misingi ya mgawanyo wa kazi kijinsia. Hali hii inajionyesha katika mila za makabila mbalimbali wakati wa sherehe za jando na unyago, katika mitaala ya elimu, sera za serikali na sheria za nchi na matoleo ya habari. Kuendeleza tabia na matendo yanayofuata misingi ya mgawanyo wa kazi kijinsia inachangia kuimarisha mila na desturi. Kwa mfano, imani zilizopo kwamba watoto wa kiume ndivyo wanaweza masomo ya hesaabu na sayansi kuliko wasichana . Imani kama hizi pia zimejengwa kwenye mgawanyo wa kazi zinazodhaniwa kwamba ni za wanawake kama kazi za uuguzi , ualimu, wasichana wanapolea wadogo zao. Kazi kama hizi kwa wastani zinatoa malipo kidogo sana na madaraka kidogo sana kwa wasichana. Lakini kwa upande wa wavulana masomo wananayosoma yanawawezesha kuendeleza kazi za jadi, kwa mfano kuwa viongozi na watu wanaotoa maamuzi , kuwa wanasiasa , kazi zinazowapatia nafasi ya kutumia madaraka.
Mbinu za uwezeshaji sehemu ya kwanza.
Jinsi na Jinsia:
Washiriki kubungabongo wanavyoelewa jinsi na jinsia.
Kazi za kijinsia
Kila mshiriki achore picha ya wanawake/wasichana; wanaume/wavulana wakifanya kazi mbalimbali wanazotarajiwa na jamii kwamba ndiyo kazi aidha za wanawake au za wanaume michoro yote ibandikwe ukuta wa pembeni.
Mahitaji ya kijinsia.
Mwezeshaji atoe maelekezo mafupi.
" Kila mmoja wenu atapewa zawadi kwa kuhudhuria semina hii. Tafakari kwa uangalifu andika kwenye karatasi hitaji lako muhimu ambalo ungependa uzawadiwe kwao"
Mnapojadili na kuchambua majibu yaliyotolewa , tenganisheni mahitaji ya wanawake na wanaume . Jadilianeni kuhusu mahitaji hayo. Aidha mahitaji hayo yapangwe katika makundi mawili:
Kundi la kwanza - Lenye mahitaji ya muihmu kwa kazi za kila siku.
Kundi la pili - Lenye mahitaji mbinu.
Kujenga uhusiano wa kijinsia inaaminika namna ambavyo mgawanyo wa kazi , tabia na mgawanyo wa rasilimali vilivyogawanywa kwa makusudi, kupangwa kwa utaratibu maalum na kupenyezwa katika fikra na mawazo ya wanawake kwa muda mrefu kulingana na misingi ya vikundi na wanaume vilivyopo katika jamii zetu. Vikundi hivi vinajumuisha familia, shule, kijiji, dini na habari katika maeneoya kazi.
Familia.
Familia nyingi zinapenda kupata mtoto wa kiume kuliko kupata mtoto wa kike kwa sababu ya wajibu wake katika kuendeleza ukoo. Katika jamii zingine kuzaliwa na kuita jina kwa mtoto wa kiume kunapokelewa kwa sura tofauti na inavyokuwa kwa mtoto wa kike.Vilevile mara moja mtoto anapozaliwa wanaanza kuashiria kazi atakazozifanya anapokuwa mtu mzima. Kwa mfano, ili kuonyesha mtoto wa kike atafanya kazi za nyumbani , mzigo wa kuni unawekwa pembeni yake, mtoto wa kiume anatarajiwa kuwa mlinzi, mkuki huwekwa pembeni yake. Elimu ya unyago na jando, mazoea ya ndoa, na elimu ya kisasa vinajenga misingi ya kuonyesha tunataka wanawake na wanume wafanye kazi aina gani hapo baadaye.
Ngazi ya kijiji au jamii.
Kwa kawaida katika kijiji au jamii watu huishi pamoja aidha katika familia moja au makundi yenye familia kadhaa . Mara nyingi watu hawa huwa wana uhusiano wa karibu kutokana na historia yao , mila , desturi, utamaduni wao, njia zao za kiuchumi, kisiasa na hali ya kuthamini utu vinafanana. Kufuatana na ukweli wa kihistoria , jamii nyingi zimekuwa zikitoa mafunzo kwa wavulana na wasichana wanapofikia umri wa kubalehe.Wanaume watu wazima hutoa mafunzo kwa wavulana kuwaelekeza wajibu, majukumu na nafasi yao katika familia na jamii kwa ujumla, hususan kuwa na sauti na madaraka juu ya wanawake. Vilevile wanawake watu wazima wanawafundisha wasichana wajibu, majukumu na nafasi yao katika kaya na jamii ni kuwa chini ya amri na madaraka ya wanaume bila kuuliza, kulalamika au kukataa chochote kinachomtokea. Mbinu za mafunzo haya zilijumuisha nyimbo, ngoma, dansi za asili, ngonjera zikiwa ndizo njia kuu za mawasiliano.
Hapa Tanzania jamii zetu zimejengwa kwenye misingi ya mifumo ya aina mbili. Wa kwanza ni mfumo dume ambao unawapatia upendeleo wanaume wanapewa nafasi ya kwanza wanaonekana wao ni muhimu kuliko wanawake. Wao hukabidhiwa nafasi za maamuzi na madaraka juu ya wanawake; kumiliki mali na rasilimali za familia na ukoo ikiwemo ardhi. Malezi na makuzi ya watoto wa kiume imejengwa katika misingi hii.
Aina ya mfumo wa pili ni ya mfumo jike ambapo wanawake watu wazima wanakuwa na maamuzi kuhusu watoto wao na kurithi mali lakini madaraka ya kuamua yako mikononi mwa wajomba.
Aidha utendaji wa kazi za kujitolea katika ngazi ya kijiji au jamii kati ya wanawake na wanaume umejengwa kwenye misingi ya mgawanyo wa kazi kijinsia ambao wanawake hufanya kazi zisizo na malipo pia hazipewi thamani inayostahili. Wanaume wachache hufanya kazi zenye malipo na vilevile wanaume ndio wanashiriki katika shughuli za kisiasa na kufanya maamuzi.
Shule/Elimu
Kama ilivyo sehemu katika zote duniani, elimu huimarisha makuzi na malezi yaliyofundishwa ngazi za kaya na jamii . Kuna mambo kadhaa yanayochangia kuimarisha uhusiano wa kijinsia:-
Dini.
Dini na imani ni mojawapo ya taasisi zinazoendeleza misimamo mikali ya mfumo dume na tofauti za kijinsia. Imani za uumbaji na namna ambavyo kazi za kijinsia zinavyoangalia suala zima la hatima ya ubinadamu zinajenga mahusiano haya. Kwa mfano katika madhehebu ya wakristo yaliyo mengi wanawake ni kati ya waaumini walio wengi wanaoenda makanisani kusali ukilinganisha na wanaume lakini wanaume ndio wanaoshika nafasi za uongozi katika makanisa. Kwa kutumia jina la dini, wanawake wanaonekana ndio chanzo cha kufanya mwanadamu afanye dhambi kama inavyojionyesha katika kielelezo hiki.
" Tangu ulipoanguka katika bustani ya Eden , mwanamke ni binadamu mwenye matatizo, hata Yesu hakuwaamini wanawake vinginevyo angekuwa na mitume wanawake ."
Vyombo vya habari.
Vyombo vya habari vinachangia kujenga na kuimarisha mfumo dume kwa kuonyesha ambavyo wanaume wapo kwenye nafasi za juu na madaraka wakati wanawake wapo kwenye nafasi za chini na za kukandamizwa. Hivi karibuni matangazo mengi ya mafuta ya kupikia na sabuni za kufulia yamekuwa yakidhihirisha hali hii kwa kuonyesha wanawake ndiyo wahusika wakuu katika kazi za kupika na kufua katika kaya, wakati mwingine mikakati ya kujenga na kuimarisha uhusiano wa kijinsia inatengenezwa kwa njia ambayo inawarubuni wanawake hivyo inakuwa vigumu kwa wao kutambua kwamba wananyanyaswa.
Jinsia na Ajira rasmi.
Namna ambavyo mgawanyo wa kazi kijinsia unavyotekelezwa na kuimarishwa kwenye ngazi ya kaya na jamii, ndivyo hivyo unavyotekelezwa hata kwenye taasisi za ajira rasmi. Aidha sehemu hizi zinachangia kujenga misingi ya ubaguzi wa kijinsia katika sera, taratibu na sheria za ajira. Mara nyingi wanaume wanashika nafasi za juu za kuongoza na kutoa maamuzi , kazi zenye kutoa ujuzi na zinalipa mishahara na masilahi makubwa. Wanawake walio wemgi wanafanya kazi za hadhi ya chini, mishahara midogo na ujuzi kidogo. Pia wafanyakazi wanawake katika ngazi hizi hutumika kuwahudumia mabosi wao ambao ni wanaume katika huduma za chai na kadhalika kuna wanaume wachache sana sana ambao ni wachapa mashini, kuwahudumia mabosi.
Uhusiano uliopo kati ya wafanyakazi wanawake na wafanyakazi wanaume ni kama inavyojionyesha hapo chini.
| Wafanyakazi wanaume | Wafanyakazi wanawake |
| Meneja Daktari Mwanasayansi Mhandisi Msanifu majengo Mhasibu Rubani |
Katibu Muhtasi Muuguzi Mhudumu wa Maabara Fundi mchundo Mchoraji wa ramani Karani Mhudumu wa kike |
Maendeleo yanahusu mabadiliko siyo katika maisha ya watu peke yake bali pia katika hatua mbalimbali zinazowawezesha wanawake na wanaume kufanya shughuli za kujiletea mabadiliko ya kuinua hali zao za maisha. Dhana ya jinsia na maendeleo ina maana ya kwamba:-
Inabidi ieleweke kwamba jinsia ni sehemu ya maendeleo kwa hali hiyo masuala ya jinsia lazima yaonekane bayan katika mipango yote ya maendeleo. Mipango hii inapoandaliwa inabidi izingatie ukweli kwamba wanawake na wanaume ndiyo washiriki wakuu katika kuleta maendeleo, majukumu na wajibu wao hutofautiana . Kwa hali hiyo mahitaji yao ya kijinsia pia yanatofautiana . Kwa hali hiyo mipango ya kijinsia inabidi ilenge kila kundi.
Kutambua masuala ya kijinsia katika maendeleo.
Jinsia inaelezwa kama:-
Ubaguzi wa kijinsia unaibua mapungufu ya kijinsia katika maendeleo ambayo yanatokana na tofauti kati ya wanawake/wasichana na wanaume/wavulana zilizojengwa kwenye mila na desturi, sera na sheria.
Ubaguzi katika hatua ya familia au jamii unaweza usiungwe mkono na sheria ya nchi lakini mila zinaweza kuamuru na ikakubalika. Kwa mfano upendeleo kwa mvulana kwenda shule, kula vizuri na kucheza.
Uongozi na usimamiaji unaweza kubagua jamii dhidi ya wanawake. Taasisi za serikali mara nyingi bila sheria za msingi hukataa kujenga uwezo wa wanawake. Kwa mfano kukataa kutoa mikopo kwa wanawake,kutowashirikisha wanawake, kukataa kuwaruhusu wasichana kurudi shule baada ya kujifungua. Kwa upande mwingine sheria za nchi zinaweza kukandamiza, kwa mfano kuwakatalia wanawake katika aina fulani za kazi. Mara nyingi sheria za nchi zinatoa haki katika maandishi lakini katika hali halisi haki hizi hazipatikani.
Mapungufu ya kijinsia.
Hii inatokea panapo mgawanyo katika kazi za kijinsia usio sawa katika mzigo wa kazi, mali na rasilimali, nafasi za masomo, mafunzo na fursa zingine.Matokeo ya tofauti hizi za kijinsia husababisha mapungufu ya kijinsia kupatikana.
Mojawapo ya jitihada za wanawake kumaliza ubaguzi, wanawake wazingatie njia zinazowawezesha kugundua tofauti za kijinsia zilizojengwa katika jamii ambayo huendeleza mwanaume kuwa katika nafasi ya juu . Juhudi hizi huongeza kujenga uwezo wa mwanamke.
Mbinu za uwezeshaji : Jinsia na Maendeleo.
Malengo ya somo.
Ifikapo mwisho wa somo hili washiriki waweze :-
Maelezo kwa washiriki.
Mjadala.
Wagawe washiriki katika makundi mawili.: Kundi A - Linakubali
Kundi B - Linakataa
Muda ( Dakika 30)
Mbinu za uwezeshaji: Mchezo wa Kujenga Mnara.
Wagawanye washiriki makundi mawili yenye idadi sawa ya wanaume na wanawake , kila kundi lipewe vitu vilivyo sawa wavitumie kujenga mnara.
Kila kikundi kitumie dakika kumi kujenga mnara. Kila kundi liwe ni mtu anayeangalia mambo yanayofanyika lakini zaidi achunguze:-
Baada ya kazi ya makundi na wawakilishi ( waliokuwa wanaangalia) kuwasilisha, mwezeshaji aulize maswali machche kuhusiana na mrejesho;
Hitimisho:
Maendeleo siyo kuleta mabadiliko ya maisha ya watu tu bali pia ni katika hatua mbalimbali zinazochukuliwa na wanawake na wanaume kuleta mabadiliko haya.
Haki za binadamu ni lazima kwa wanaume na wanawake. Haki hizi zimetajwa wazi katika matamko mengi, mikataba ya kimataifa, kikanda na katiba ya nchi ambayo mwaka 1984 iliingiza Tamko la Mkataba wa Haki za Binadamu lililopitishwa Umoja wa Mataifa mwaka 1948.
Haki za binadamu za wanawake zinajadiliwa kwa sababu wanawake hawajawa kwenye nafasi na fursa sawa kama ya wanaume. Wao bado wananyanyaswa na kukandamizwa na kuonewa na mifumo ya maisha iliyopo. Haki za binadamu za wanawake ni pamoja na haki za kiutamaduni, kiuchumi, kijamii, kisiasa na haki za kiraia. Masuala yanayoashiria wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuwepo mgawanyo mzuri wa kazi kijinsia na rasilimali, hali ambayo kwa sasa hivi haipo.Vilevile inatokana na kutambua kwamba haki za binadamu za wanawake na wasichana hazijatekelezwa kama katiba ya nchi yetu na mikataba ya kimataifa inavyotaka ifanyike.
Mtizamo wa kutumia dhana ya haki za binadamu katika maendeleo unaleta changamoto ya kuwafanya wanawake wasionekane kama vile wanasubiri kuletewa maendeleo na kunufaika na sera za maendeleo , bali kulenga nyenzo na rasilimali kwa wanawake , kujenga uwezo wao na kwa hali hiyo kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake. Mtizamo wa haki za kibinadamu katika maendeleo utawezesha jamii mbalimbali kufanya bidii ili kufikia usawa wa kijinsia.
Mwaka 1979 Umoja wa Mataifa uliidhinisha Mkataba wa Kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake .Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliridhia mkataba huu mwaka 1985. Licha ya kuridhia mkataba huu, serikali pia imeridhia mikataba mingi ya Umoja wa Mataifa , Kikanda inayolenga kuleta usawa kijinsia. Vile vile haki hizi zimetajwa kwenye katiba yetu ambayo ndiyo sheria mama,